Luke 16:29-31

29 a“Ibrahimu akamjibu, ‘Ndugu zako wana Torati ya Musa na Manabii, wawasikilize hao.’

30 b“Yule tajiri akasema, ‘Hapana, baba Ibrahimu, lakini mtu kutoka kwa wafu akiwaendea, watatubu.’

31“Ibrahimu akamwambia, ‘Kama wasipowasikiliza Musa na Manabii, hawataweza kushawishika hata kama mtu akifufuka kutoka kwa wafu.’ ”
Copyright information for SwhKC